SHILAWADU YAWAPAMBANISHA SINGELI NA BONGO FLEVA MANZESEWASANII wa muziki wa kizazi kipya na muziki wa singeli -Msaga Sumu, Dulla Makabila, Shilole, Edu Boy na Pink, Jumamosi Mei 6, watapanda kwenye jukwaa moja katika onyesho maalum la Shilawadu, litakalofanyika kwenye JM Night Club Manzese Jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa onyesho hilo Soud Brown, alisema kuwa onyesho hilo la maalum la kipekee limepelwa Mazense kwa lengo la kutoa burudani kwa wakazi wa eneo hilo.

Alisema kuwa wana amini kila msanii waliyemchukua atatoa burudani ya aina yake kwa wakazi wa mazense, ambao hawajawahi kupata muunganiko huo.
"Nikiwa kama mratibu, nina amini kila mpenzi atakayepata nafasi ya kuja kwenye onyesho letu atapata burudani ya kutosha kutoka kwa kila msanii tuliyemchukua maana wote ni wasanii wazuri na wana nyimbo zinazopendwa na kila mpenda muziki hapa nchini", alisema

No comments