SHIMMUTA YAJIPANGA KWA MCHAKATO WA MASHINDANO YAJAYO

SHIRIKISHO la michezo ya mashirika ya umma makampuni ya taasisi binafsi (SHIMUTA) limesema kuwa Kamati ya Utendaji ipo kwenye mchakato wa kukamilisha jukumu la kupata mwenyeji wa mashindano ya mwaka huu.

Jukumu hilo lilitolewa na wajumbe wa mkutano huo katika mkutano mkuu ambao ulishindwa kupata muafaka wa mkoa mwenyeji wa michezo ya mwaka huu.

Akizungumza na saluti5 Katibu mkuu wa SHIMMUTA, Award Safari alisema kuwa harakati za kukutana kwa kamati hiyo zinafanyika ili kupata mwafaka kwa mkoa utakaopitishwa kuanza kujipanga.

Alisema mikoa iliyowekwa katika kinyang’anyiro hicho ni pamoja na Mwanza, Morogoro na Moshi mkoani Kilimanjaro.

Safari alisema kitakachoangaliwa ni mkoa kama una vipaumbele vya huduma muhimu na za karibu ili kuwezesha washiriki.

“Tunachokifanya sasa ni kamati yetu kukutana tuweze kufikia mwafaka na tuweze kufikia mwafaka na tuweze kuwasilisha kwa wajumbe wa mkutano kile kitakachojiri,” alisema Safari.

Alibainisha vitu vinavyo hitajika ni pamoja na huduma za muindombinu bora hususan viwanja vya michezo, hoteli kwa ajili ya washiriki na urahisi utakaowawezesha washiriki katika kituo cha mashindano na vingine vingi.

No comments