ZIKIWA zimebaki siku 10 tu kabla ya pambano la mahasimu wa jadi, Mlimani Park Sikinde na Msondo Ngoma Music Band, majigambo yameonekana kupamba moto ambapo Sikinde wamedai watawatoa nishai wapinzani wao hao.

Kiongozi mwandamizi na mwimbaji kiraka wa Sikinde, Abdallah Hemba ameongea na saluti5 na kusema kuwa, anafahamu kwamba ndani ya Msondo kuna ndugu zake wawili ambao ni Athumani Kambi na Juma Katundu, lakini siku hiyo udugu watauweka pembeni kwa muda.

“Hiyo siku itakuwa ni yetu kwa ajili ya kujenga historia ambayo haitakaa ifutike kwa upande wa muziki kwani tutaonyesha kazi kubwa vitakavyowasambaratisha wapinzani wetu,” amesema Hemba.


Hemba amesema kuwa, vipo vitu vipya watakavyovifanya ghafla ukumbini kama “surprise” ikiwemo vibao vipya ambavyo anaamini vitazidi kuwadhoofisha Msondo Ngoma.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac