SIKU YA HUKUMU CHOCKY, MUUMIN, NYOSHI YAWADIA …ni El Clasico ndani ya Escape One Ijumaa hii


Waimbaji magwiji wa dansi Ally Chocky, Mwinjuma Muumin na Nyoshi el Saadat wanapambanishwa kwenye jukwaa moja Ijumaa hii Mei 19 jijini Dar es Salaam.

Onyesho hilo lililopewa jina la ‘Magwiji El Clasico’ litafanyika ndani ya ukumbi wa Escape One, Mikocheni ambapo kila mmoja atapigiwa na 'live band'.

Mratibu wa onyesho hilo Dj Elly wa Clouds FM, ameiambia Saluti5 kuwa onyesho hilo limeandaliwa ili kumaliza ubishi miongoni mwa waimbaji hao ambao kila mmoja anatamba kuwa ndiye mfalme wa dansi la kisasa lililofanyiwa mageuzi makubwa mwishoni mwa miaka ya 90.

Dj Elly amesema onyesho hilo litasindikizwa na Khadija Kopa, Msagasumu, MC Soud na Madada 6 huku kiingilio kikitajwa kuwa ni sh. 15,000 na 25,000 kwa V.I.P.

No comments