SIMBA YATAMBIA UDHAMINI WA SPORTPESA... sasa yasubiri udhamini mwingine kutoka Juventus

SIMBA imeingia udhamini wa kufuru wa zaidi ya sh bil 4.9 na kampuni ya kubashiri matokeo ya soka ya Sportpesa ambayo pia inadhamini baadhi ya timu za Ligi Kuu ya England na Kenya.

Ijumaa katika uwanja wa taifa baada ya kipindi cha kwanza kumalizika cha Ligi Kuu kati ya Simba na Stand United, wachezaji wa Simba waliingia katika kipindi cha pili wakiwa wamevaa jezi zenye nembo hiyo.

Baadaye akiongea na waandishi wa habari, rais wa Simba, Evans Eveva alisema kwamba udhamini huo utakuwa na manufaa makubwa kwa Simba.

Mkataba huo, itaifanya Simba ipokee kitita cha sh mil 888 katika mwaka wa kwanza.

Mmoja wa wakurugenzi wa Sportpesa, Abbas Tarimba amesema Simba itapewa sh bil 1 na mil 80 katika mwaka wa mwisho wa mkataba kwa kuwa kila mwaka, asilimia 5 ya fedha zitakuwa zinaongezeka katika mkataba.

Kama hiyo haitoshi, Simba imepewa motisha kuwa kama atachukua ubingwa basi ina nafasi ya kuchukua sh mil 100 kama zawadi au pongezi kutoka Sportpesa wameonyesha wanachotaka ni Simba kufanikiwa kweli, wametenga sh mil 250 wakibeba Kombe la Kagame au michuano iliyo chini ya Caf.

Aveva amesema kwamba udhamini huo unakuwa ndiyo mkubwa zaidi kuliko mingine yote ambayo Simba imewahi kuingia kudhaminiwa.

Mkataba huo unaifanya Simba kuwa timu isiyo na hasara kama ilivyo kwa msimu huu ambao imemaliza ikicheza bila ya kuwa na udhamini mkuu.

Licha Sportpesa, Simba imekuwa pia ikidhaminiwa na mfadhili wake Mohamed Dewji “MO” lakini pia inajiandaa kupokea udhamini wa ushirikiano kutoka klabu marufu barani Ulaya, Jeventus na Italia.

Mo amefanya mazungumzo ya awali na Juventus alipokuwa kwenye shughuli zake za kibiashara nchini Italia na ameahidi kwamba watemi hao wa soka barani Ulaya watakuja kukamilisha mazungumzo na Simba wakati wowote.

No comments