SIMON MSUVA AZIDI KUPANDIWA DAU UARABUNI

NEEMA kubwa inazidi kumshukia mshanbuliaji wa Yanga Simon Msuva baada ya klabu ya Al Ettihad kumfuata lakini sasa klabu kongwe ya Zamalek nayo imetua kutaka huduma ya mshambuliaji huyo.

Wakati Yanga ikijadiliana juu ya Ofa ya sh mil 150 za klabu ya Ettihad ya Misri, wakala mwingine ametua Jangwani akiweka mambo mazuri mapya juu ya Msuva kutakiwa na Zamalek ambao wameongeza ofa kubwa mezani tofauti na Ettihad.

Zamaleki katika ofa hiyo, wametaka kuipa Yanga sh mil 180 kwa winga huyo mwenye uwezo mkubwa wa kufunga, ofa ambayo Yanga italazimika kuumiza kichwa kwa kupiga hesabu wapi sehemu sahihi kwa kuuzwa mshambuliaji huyo.

Msuva bado amebakiza mkataba wa mwaka mmoja na Yanga ambapo mabosi wa timu hiyo wanataka kuziwekea kikosi maalum ofa hizo lakini pia watamvuta Msuva mezani naye kuchangia mawazo katika madili hayo.

“Unajua tulikuwa tunajua kwamba Ettihad ndiyo waliojitokeza mbele kumuhitaji Msuva lakini wakati hilo likitafutiwa ufumbuzi, Zamalek nao wametuma ofa yao na tunaijadili sasa,” alisema bosi huyo wa Yanga.

“Zamalek wamesema wazi na wako tayari kutoa kiasi cha zaidi ya hicho cha Ettihad na walichovutiwa ni uwezo wa  Msuva katika kutengeneza mashambulizi na kufunga mabao."

No comments