SIMON MSUVA: TUNAWANGOJA KWA HAMU MBAO FC

PAMOJA na kupata jeraha wakati wa mchezo dhidi ya Mbeya City kwenye dimba la uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, winga wa Yanga, Simon Msuva amesema kuwa bado akili yake inafikiria mchezo wao wa mwisho dhidi ya Mbao FC.

Winga huyo alisema kuwa ni nafasi yao pekee kwenda kulipa kisasi kwa Mbao FC ambao waliwatungua na kufanikiwa kutinga hatua ya fainali ya Kombe la FA.

Msuva aliukosa mchezo wa Jumanne dhidi ya Toto Africa ya jijini Mwanza lakini anatarajia kuwepo uwanjani kwenye mchezo dhidi ya Mbao FC.

“Ndio. Tulipoteza mechi kwa sababu ya kimchezo, lakini Mbao watarajie kukutana na kitu cha tofauti kabisa, ni lazima tuendelee kulinda ukubwa wa jina la Yanga,” alisema Msuva.

Simon Msuva amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu tangu kukosekana kwa Donald Ngoma, amekuwa msaada mkubwa kwa timu kutokana na mabao muhimu anayofunga.

No comments