SIZA MAZONGELA AFIWA NA MAMA YAKE MZAZI …mazishi leo saa 10


Mwimbaji nyota wa miondoko ya segere na taarab, Siza Mazongela (pichani juu) amefiwa na mama yake mzazi.

Mama yake Siza amefariki jana Jumanne usiku na atazikwa leo Jumatano Mei 10, 2017.

Kwa mujibu wa mdogo wake Siza, Haji Mazongela msiba uko nyumbani kwa Siza, Tabata Shule jijini Dar es Salaam.

Haji ameiambia Saluti5 kuwa mama yao atazikwa Kiwangwa, Bagamoyo saa 10 alasiri, ambapo msafara wa kutoka Tabata kulekea Kiwangwa utaondoka saa 6 mchana.

No comments