SOBA HOUSE YATOA USHAURI WA BURE KWA WASANII NA WANAMICHEZO KUHUSU DAWA ZA KULEVYA

UONGOZI wa kituo cha kulelea wahanga wa dawa za kulevya cha Soba House kilichopo Kigamboni, jijini Dar es Salaam kimeshauri wanamichezo na wasanii kuzingatia miiko ya fani yao kwa kukazania mazoezi badala ya kuamini katika ulevi, anasa na uchawi.

Akiongea na saluti5, bosi wa kituo hicho, Pili Soba amesema kuwa wasanii na wanamichezo wengi wanajiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya kwa kufuata mkumbo na matokeo yake kujikuta wakiharibikiwa.

“Wasanii na wanamichezo wetu wengi hawaamini katika kujituma na kufanya mazoezi kwa bidii, wao hudhani zaidi uchawi na ulevi, kwamba wanahisi wanapotumia labda bangi na dawa nyingine za kulevya ndipo wanapata nguvu,” amesema.

“Matokeo yake dawa hizo huwaharibu kwa kuwamaliza nguvu na kuwafanya wawe dhaifu kiasi wanashindwa kumudu kuwika kwa muda mrefu katika fani zao,” ameongeza bosi huyo.


Amewashauri wanamichezo na wasanii kuzidisha bidii katika ufanisi na kuacha kujitumbukiza kwenye makundi yasiyofaa ambayo matokeo yake huwashawishi mambo maovu yanayokuja kuua na kuteketeza vipaji vyao. 

No comments