SPORTPESA YABORESHA MKATABA WAKE WA UDHAMINI NA KLABU YA SIMBA

KAMPUNI ya michezo ya kubahatisha ya SportPesa imeuboresha mkataba wa udamini na klabu ya Simba na kuongeza kiasi cha udhamini.

Habari ambazo saluti5 imezipata zinasema kwamba uamuzi wa kampuni hiyo yenye makao yake makuu nchini Kenya umekuja kwa kuzingatia ukubwa wa Simba na jinsi timu hiyo inavyoungwa mkono na wanachama wake.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Simba zimeeleza kwamba mkataba huo utaboreshwa kutoka kikita cha sh mil 888 kwa mwaka hadi sh mil 950.

“Ni kweli mkataba tulioingia mwanzo sasa umeboreshwa kutoka sh bil 4.9 kwa miaka yote mitano hadi sh bil 5.173,” kilieleza chanzo cha uhakika kutoka ndani ya klabu hiyo.

“Unajua wale jamaa wa Sportpesa ni welevu sana, mkataba huu baada ya kuboreshwa utakuwa sawa kwa sawa kabisa na watani wetu Yanga.”

Sportpesa wamefanya hivyo kuondoa malalamiko kwamba Yanga mkataba wake ni mnono zaidi ya ule wa Simba wakati timu zote zina hadhi sawa na kwamba sasa timu zote zinapata kitita sawa katika mkataba huo.

Hivi karibuni baada ya Simba kusaini mkataba mpya kulizuka tafrani hadi za Zacharia hans Poppe akatangaza kujiuzulu kwenye Kamati ya Utendaji na uenyekiti wa kamati ya Usajili.

Hata hivyo, baadae Hans Poppe alizungumza na viongozi wa Simba waliomwomba arejee tena.

Pia kulikuwa na sintofahamu kati ya viongozi wa Simba na wanachama na mfadhili wao, Mohammed Dewji ambaye pia aliamua kujiweka kando akiwa na madai sawa na yale ya Has Poppe, lakini jana imetangazwa kwamba amerejea kuendelea kuisaidia Simba.

No comments