SPOT PESA YAPELEKA NEEMA YA UDHAMINI JANGWANI

YANGA neema kubwa imewashukia baada ya kupata udhamini mkubwa ambao utamaliza karibu mambo mengi ya ukata uliokuwa ukiikumba klabu hiyo na sasa ghafla wamegeuka mabilionea.

Udhamini ambao umetua yanga ni ule wa sport pesa ambao utaipa Yanga kiasi cha zaidi ya sh. bil 1 za Kitazania na kuleta furaha kubwa Jangwani wakati huu klabu hiyo ikipiga hesabu za kuingia katika zoezi la usajili katika kuelekea msimu ujao.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga ni kwamba dili la udhamini huo limekamilika rasmi baada ya kutimia zaidi ya mwezi mmoja wa mazungumzo kabla ya kukamilika katika kikao cha Kamati ya utendaji cha klabu hiyo.

Sport pesa ambayo pia ndiyo wadhamini wa klabu kubwa ya Hull City ya England awali iliitaka kuidhamini Yanga kwa kiasi cha sh mil 750 lakini Yanga ikagomea na kiasi hicho kupanda mpaka kufika billioni moja ya Kitanzania.

Ndani ya mkataba huo wa mwaka mmoja Yanga itanufaika na mambo mengi yakiwemo pia klabu kupatiwa basi kubwa la kisasa litakaloletwa kwa ajili ya timu hiyo pamoja na kukarabatiwa kwa uwanja wa Kaunda.

Sambamba na hilo pia kampuni hiyo itachangia kiasi cha fedha katika usajili wa msimu ujao na kila kitu kimekamilika likibaki zoezi la kusaini mkataba huo ambalo huenda likafanyika kesho katika hafla maalumu makao makuu ya Yanga mitaa ya Jangwani an Twiga


“Jana mkataba huo ulikuwa kwa wanasheria wa klabu akipitia kabla ya kufanyiwa maboresho ya mwisho na kama kila kitu kitakamilika salama huenda Jumanne kesho tukakamilisha kwa kusaini mkataba huo,” alisema mmmoja wa wajumbe wa Kamati ya utendaji wa klabu hiyo.

No comments