STAA WA FILAMU NOLLYWOOD AOTA MAFANIKIO YA HOLLYWOOD NCHINI MWAO

STAA wa Nollywood, Toyin Abraham amesema kuwa anaona kuna uwezekano mkubwa kiwanda chao cha filamu kikafikia hatua waliofikia Wamarekani kupitia filamu za Hollywood.

Toyin alisema kuwa filamu za Nigeria tayari zimefanikiwa kuteka soko la Afrika na hatua inayofuata ni kuzivusha nje ya bara hili.

“Naona inawezekana kabisa tukafika hatua ya Hollywood kwa miaka kadhaa ijayo, naamini hivyo kwasababu soko tumefanikiwa kuliteka,” alisema staa huyo.


Staa huyo alisema hayo alipokuwa sambamba na mzalishaji wake Patrick Doyle wakati walipokuwa kwenye kongamano la filamu nchini Nigeria.

No comments