STAMINA ATOA USHAURI WA BURE KWA SERIKALI KUHUSIANA NA SOKA LA BONGO

STAMINA mbaye ni mkali wa bongofleva ameishauri serikali kuuangalia mchezo wa soka kwa jicho la tatu ili kutoa hamasa kwa vijana kuingia kwa wingi kwenye mchezo huo na kuepuka taifa kuendelea kuwa “kichwa cha mwendawazimu”.

“Imefika wakati sasa serikali itilie mkazo zaidi kwenye soka letu ili muda mwingine nasi tujikute tukitoka kimasomaso badala ya kila siku kuwa wasindikizaji tu na kushika mkia kwenye michezo,” amesema Stamina.


Stamina amesema kuwa ni vyema ingewekwa mikakati kwa wizara yenye dhamana kuwaweka vijana sehemu moja na kuangalia namna ya kuwatia motisha kwa ajili ya maslahi ya soka la Bongo.

No comments