Habari

TAARIFA YA KUJIUZULU KWA MANJI YAZUA SINTOFAHAMU KWA MASHABIKI WA YANGA

on

WANACHAMA
na wapenzi wa Yanga wamepatwa na mishtuko mkubwa baada ya taarifa kuzagaa
kwamba mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji amejiuzulu nafasi yake hiyo.
Mei 23, mwaka huu kulikuwa na barua iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha kuwa
Manji ameachia uenyekiti wa klabu ya Yanga na makamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Clementi Sanga atakaimu.
Wanachama
na wapenzi hao waliongea na saluti5 kwa nyakati tofauti na kutoa maoni yao kuhusu kujiuzulu kwa Manji huku wengi wakitaka aendelee
kuisaidia timu hiyo hasa katika kipindi hiki cha usajili.
Mwanachama
mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Ally Hassan kutoka jijini Dar es Salaam
alisema kwamba hana tatizo na uamuzi wa Manji lakini anachomuomba mwenyekiti
huyo ni kuendelea kuisaidia klabu hiyo kwenye usajili.
“Mimi
namuomba Manji aendelee kuisaidia timu yetu hata kama ameamua kujiweka pembeni
sababu kipindi hiki cha usajili ni kigumu sana kwetu hivyo aendelee kusaidia
timu kwenye usajili.”
Mwanachama
mwingine aliyejitambulisha kwa jina la John Haule kutoka Mbagala jijini Dar es
Salaam alisema Kwamba ameshitushwa mno na taarifa hizo lakini anachoomba ni kwa
Manji kuendelea kuisaidia timu hiyo katika usajili.
“Unajua
tuna wachezaji wa kigeni ambao wanalipwa mishahara mikubwa sana, hatutaweza kuendelea kuwalipa wachezaji hawa hivyo namuomba Manji aendelee
kuisaidia timu yetu.

Mashabiki walikuwa ni wengi waliozungumza na mtandao huu ambapo wengine walionekana kushitushwa mno taarifa hivyo na kuwekwa kwenye hali ya
sintofahamu.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *