TASMA YAITA WADAU WA MICHEZO KUWANIA NAFASI ZA UONGOZI

CHAMA cha madaktari wa michezoni Tanzania (TASMA) kinatoa wito kwa wadau wa michezo hususan wanataaluma kujitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Juni, mwaka huu.

Katibu mkuu wa chama hicho, Dk Nassoro Matuzya alisema kuwa lengo ni kuhakikisha viongozi wenye moyo na kuongoza chama wanapatikana kwa ajili ya kuendesha gurudumu la maendeleo katika sekta ya tiba michezoni.

Alisema kuwa kutokana na hali halisi kuwa katika chama hicho ni kujitolea kinachohitajika na moyo wa kuhakikisha maendeleo ya michezo inasimamiwa kwa kuwasaidia katika kuhakikisha wachezaji wanapata tiba wakiwa michezoni.

DK Matuzya alisema kuwa chama kinaendelea na maandalizi ya kuhakikisha kunakuwa na fedha ambapo wanazungumza na wadau na wafadhili ili waweze kuwasapoti.

Aliongeza kuwa nia ni pamoja na kuhakikisha wachezaji wanapata huduma bora na tiba pindi wanapopata changamoto wakiwa michezoni kwa kupata huduma ya kwanza kwa haraka zaidi.


“Kwa sasa tunachosisitiza kwa watu kujitokeza kuomba nafasi mbalimbali za uongozi ili tuweze kupata uongozi utakaofanya kazi kwa waledi kwa manufaa ya taifa kwa jumla,” alisema.

No comments