TFF KUMFUNGIA MKEMI ILI KUWAZIBA KIDOMODOMO WADAU NA MASHABIKI WA SIMBA

TAARIFA za ndani kutoka shirikisho la soka Tanzania (TFF), ni kwamba inajipanga kumfungia mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi, lakini siri ya kifungo hicho inatokana na msemaji wa Simba, Haji Manara.

Taarifa hiyo inasema kwamba, Mkemi ameitwa katika Kamati ya Nidhamu akituhumiwa kuwashambulia viongozi wa Bodi ya Ligi na Kamati ya saa 72.

Bosi mmoja wa TFF alisema Mkemi atafungiwa lengo likiwa ni kutuliza hasira za wadau wa Simba kufuatia kufungiwa mwaka mmoja na faini y ash. mil 9 aliyopewa Manara.


Alisema, lengo la hukumu hiyo ni kutuliza kelele za wadau hao katika kuacha kuishambulia TFF katika kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti, mwaka huu.

No comments