TFF "WAKATAANA" POINTI TATU ZA SIMBA... mmoja wa wajumbe akiri undava ulihusika

BAADHI ya wajumbe wa Kamati ya Sheria na haki za Wachezaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wameonekana kutupiana lawama kuhusu maamuzi ya kuipoka Simba poiti zake tatu ambazo ilizipata kutoka kwa Kagera Sugar.

Mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo amesema kwamba ameshangazwa na hatua ya Bodi ya Ligi kuiandikia tena barua Simba ikisema kwamba beki wa Kagera Sugar, Mohammed Fakhi hakuwa na kadi tatu za njano.

“Nimeshituka sana kusikia kwamba wameandika barua tena kwamba Fakhi hakuwa na kadi tatu za njano wakati barua ya kwanza ilisema alikuwa na kadi tatu. Jambo hili linatuvua nguo viongozi wote wa TFF na kwakweli ni aibu na fedheha kubwa,” amesema mjumbe huyo.

Amesema kwamba kwa bahati mbaya Simba wana barua zote na zimetoka kwenye taasisi moja, jambo ambalo wakizifikisha kwenye Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), ni aibu kwa Tanzania.

“Tuwe wakweli, tumeinyonga Simba katika jambo hili kwa maslahi ya watu wengine, sasa kama jambo hili likifika FIFA ni aibu kubwa sana kwa Tanzania. Hakuna njia nyingine zaidi ya kukaa na Simba na kuangalia mapungufu yao yako wapi,” amesema.

Mjumbe huyo amesema kwamba, yeye kama mmoja wa watu waliokuwa katika kikao cha Kamati ya Sheria kilichoirejeshea Kagera Sugar, anajua kwamba Fakhi alikuwa na kadi tatu, kwahiyo ni jambo la ajabu leo kusikia kwamba hakuwa na kadi tatu.


“Tunatakiwa kusimama kwenye ukweli kwamba suala la Simba limetokana na kanuni zetu na makubaliano yetu, kama kweli tuliamua kuirejeshea Kagera pointi zake kwa kigezo kwamba hawakulipa ada na wamelalamika nje ya muda basi tusimamie hapo,” amesema.

No comments