TIGANA AISIKITIKIA SIMBA AKISEMA HAJUI ILIKOSEA WAPI LIGI KUU BARA MSIMU HUU

WINGA wa zamani wa Yanga, Ally Yusuph Tigana amesema kuwa anashangazwa na namna ambavyo klabu ya Simba imeshindwa kutumia vizuri wigo mpana wa pointi kati yake na Yanga.

Hivi sasa inaonekana kama Simba inaomba watani wao hao wapoteze mchezo ndio wao mambo ya waendee vyema kutokana na hali halisi ya mwenendo wao katika Ligi ulivyo.

“Ni jambo la aibu kuona wanaivizia Yanga ipoteze mchezo ili wao wabebe ubingwa, haileweki ni namna gani waliruhusu pengo la pointi nne lifikiwe,”alisema Tigana.

“Msimu uliopita walienda vizuri lakini wakapoteza katika hatua za mwishoni, naona kila dalili za kurudia makosa ya mwaka jana, inaonekana,” aliongeza Tigana.

“Kwa jinsi walivyokuwa juu sikutarajia kama leo wanaweza kuchachamalia pointi za mezani kama walivyofanya, ni dalili ya kuelekea kushindwa.”


Simba ilianza vizuri kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara wakati wa mzunguuko wa kwanza ambapo walikuwa kileleni kwa jumla ya pointi nane, kabla ya mabingwa watetezi, Yanga hawajawakamata.

No comments