TIMBULO ASEMA HAAMINI KATIKA "KIKI"... asema kipaji cha muziki kwake ndio mpango mzima

MKALI wa bongofleva, Timbulo amesema kuwa haamini katika “kiki” na kwa upande wake anadhani “kiki” zinachangia kumshusha msanii kwa namna moja ama nyingine.

Hata hivyo, msanii huyo amesema kuwa huo ni mtazamo wake ingawaje wapo wasanii wanaoamini kuwa kuna mafanikio makubwa yanayotokana na “kiki” wanazofanya.

“Wasanii tunatofautiana na najua kuna wengine kwao kiki ni bonge la ishu na wanaamini huwanufaisha, siwezi kuwasemea kwa sababu nao wana mitazamo yao juu ya suala hilo,” amesema.

Timbulo amesema kuwa, katika maisha yake hajawahi kushawishika kujiingiza kwenye “kiki” kwavile anaona kipaji ndio mpango mzima kwake na sio “kiki”. 

No comments