TIMU ZA WAVU ZATAKIWA KUSHIRIKISHA VIJANA KLABU BINGWA MUUNGANO

TIMU za mpira wa wavu Tanzania Bara na Zanzibar zimetakiwa kushirikisha vijana katika mashindano ya klabu bingwa wavu Muungano yatakayofanyika mwakani.

Changamoto hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la taifa (BMT), Mohammed Kiganja.

Kiganja amesema kuwa lengo ni kuendeleza mkakati wa kuibua na kuendeleza vipaji kwa ajili ya kupat wachezaji wengi wa baadae katika timu za taifa za mchezo huo.

Pamoj na rai hiyo, pia aliviomba vyama vya mikoa kuhakikisha vinawekeza kwa vijana ili waweze kushiriki michezo ya UMISETA na UMITASHUMTA itakayofanyika mwaka huu.

“Huko katika kundi la vijana ndio kwenye hadhina ya kuibua na kuendeleza vipaji kwa ajili ya kushiriki michezo ya ndani na nje,” alisema Kiganja.

Nae mwenyekiti wa chama cha mpira wa wavu Tanzania Bara (TAVA), Augustino Agapa ametoa rai kwa wachezaji kuzingatia ushindani katika kila michuano ili uwezo wao uwe chachu ya maendeleo ya mchezo huo.


Kwa upande wake, Katibu wa msaidizi wa TAVA, Alfred Serengia alithibitisha kuwa timu ya Jeshi Stars wanaume na timu ya wanawake ya magereza zitashiriki klabu bingwa Afrika itakayofanyika mwakani.

No comments