TIWA SAVAGE ATAKA FILAMU ZA MAPENZI ZISIZUILIWE NIGERIA...asema ni vyema bodi ya filamu ipewe mwongozo wa kinachotakiwa

NYOTA wa muziki nchini Nigeria, Tiwa Savage amesema kuwa ni jambo gumu kuzuia filamu za mapenzi zisifanyike katika kipindi hiki cha ulimwengu wa utandawazi.

Savage alibainisha kuwa kinachoweza kufanyika ni kutoa mwogozo tu kwa bodi za filamu ili kuona namna gani inaweza kupunguza baadhi ya mambo yenye athari katika tamaduni za Kiafrika.

“Filamu za kimapenzi zinauzika sana kuliko nyingine zote, ni vigumu kuzizuia na hasa katika kipindi hiki cha utandawazi,” alisema staa huyo.

“Ili kulinda mila na desturi za Afrika, bodi za filamu zinaweza kupewa miongozo tu na sio kuzuia moja kwa moja zisiingie sokoni.”

No comments