TSHABALALA APONGEZWA NA WADAU KWA KUCHAGULIWA MWANASOKA BORA WA MSIMU

BEKI wa kushoto wa Simba, Mohammed Hussein “Tshabalala” amepongezwa na wadau wa soka hapa nchini kwa kuchaguliwa kuwa mwanasoka bora wa msimu katika Ligi Kuu ya mwaka 2016/17.

Shirikisho la soka nchini limemtangaza mwanasoka huyo kuwa mchezaji bora huku “pacha” wake wa upande wa kushoto uwanjani, Shiza Kichuya akiibuka na tuzo ya bao bora la msimu ambalo aliwafunga Yanga Februari 25, katika mechi ambayo Simba walishinda kwa mabao 2-1. 

No comments