UBINGWA WA LA LIGA MIKONONI MWA REAL MADRID …yapiga tena 4-1


Real Madrid kwa mechi ya pili mfululizo kwenye La Liga, wanashinda 4-1, safari hii ikiwa ni dhidi ya Celta Vigo ambapo Cristiano Ronaldo amefunga mara mbili.

Kwa matokeo hayo, Real Madrid sasa kila kitu kiko mikononi mwao ili kutwaa taji la La Liga na wanahitaji sare tu katika mchezo wao wa mwisho ili kuwa mabingwa wapya.

Mabao mengine ya Real Madrid yalifungwa na Karim Benzema na Toni Kroos wakati lile la Celta Vigo likifungwa na John Guidetti.

Iwapo Barcelona inayoshika nafasi pili itatoa sare katika mchezo wake wa mwisho, basi Real Madrid itatwaa ubingwa hata kama itapoteza mechi yake ya mwisho.

No comments