UJIO WA MAXIME YANGA WAMWEKA PAGUMU JUMA MWAMBUSI

KOCHA wa timu ya Kagera Sugar, Mecky Maxime yuko kwenye mipango ya kutua katika benchi la ufundi la Yanga.

Kocha huyo ambaye alipata mafanikio makubwaakiwa na kikosi cha Mtibwa Sugar kabla ya kuhamia timu ya Kagera Sukari ambayo ameiongoza kukamata nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu msimu huu.

Kocha Maxime anatajwa kurithi kiti cha Juma Mwambusi ambaye ni msaidizi wa George Lwandamina raia wa Zambia.
Juma Mwambusi alitokea Mbeya City misimu miwili iliyopita akichukua nafasi ya Charles Boniface Mkwasa.

Akiwa kwenye benchi la ufundi la Yanga amefanikiwa kuipa klabu hiyo mataji mawili ya Ligi Kuu Tanzania Bara na ubingwa wa Kombe la FA mwaka jana.

Taarifa zilizoenea ni kuwa kocha mkuu wa Yanga anavutiwa na uwezo wa Maxime aliyeiongoza timu ya Kagera Sugar kusimama juu ya Azam kwa kukamata nafasi ya tatu.


Maxime ameshawahi kuiongoza timu ya taifa kwa mafanikio makubwa akiwa nahodha mpaka anastaafu kucheza soka.

No comments