UNAFAHAMU KUWA REGINALD MENGI ALIMFUATA MZEE JANJA NYUMBANI KWAKE KUMSHAWISHI KUIGIZA ITV?... SOMA HAPA


LICHA ya kwamba marehemu Hamis Tajiri “Mzee Janja” ndie aliyekuwa miongoni mwa wasanii wa kwanza kufanya maigizo ya runingani hapa nchini, lakini pia imefahamika kuwa ndiye pekee aliyefuatwa nyumbani kwa heshima zote na bosi wa IPP, Reginald Mengi kwenda kumshawishi kupiga mzigo katika kituo cha ITV.

Hayo yameelezwa na binti wa msanii huyo, Rehema Tajiri ambaye amesema kuwa, Mzee Janja hakuamini macho yake pale Mengi aliposimamisha gari lake la kifahari barazani kwao na kubisha hodi ndani kwenda kumshawishi kuanzisha michezo kwenye runinga yake.

“Nakumbuka baba alitusimulia baada ya Mengi kuondoka kuwa wakati wote wa mazungumzo ya alikuwa anatetemeka kwa kuwa ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuzungumza ana kwa ana na mtu tajiri kama yeye,” amesema Rehema ambaye kwa upande wa soka ni shabiki wa Yanga na Manchester United.


Rehema amesema kuwa anakumbuka baada ya kikundi cha mzee Janja kilichokuwa pia kinakusanya nyota kadhaa akiwemo mkongwe mwenzie, Ibrahim Raha “mzee Jongo”, ndipo walipokuja kuibuka wasanii wengine akiwemo mzee Onyango.

No comments