VICTOR NKAMBI: ETI MUUMIN AMWAJIRI CHOCKY!? NJOZI ZA MWAKA 47, KWA UWEZO UPI? KWA BENDI IPI?


Mpapasa kinanda wa African Stars “Twanga Pepeta” Victor Nkambi (pichani juu) amemtaka mwimbaji Mwinjuma Muumin aache kuota ndoto za mwaka 47.

Victor ameyasema hayo baada ya Muumin kuwaponda baadhi ya wanamuziki wa Twanga kwa kusema wana roho mbaya na wanamnyanyasa Ally Chocky na hivyo yuko tayari kumwajiri Chocky kwenye bendi yake ya Double M Plus.

Akiongea na Saluti5 Jumamosi usiku Victor akasema: “Mwambie swahiba wako aache kuota ndoto za mwaka 47. Hivi Muumin anaweza kumwajiri Chocky? Kwa bendi ipi na kwa uwezo upi?

“Muumin ana mfano wa bendi tu, hakuna bendi pale, hana uwezo wa kumwajiri Chocky na hata kiuwezo wa kimuziki hamfikii Chocky. Mwambie apunguze kusema sema ovyo, watu watamdharau”.

Wakati Victor akisema Muumin hafikii uwezo wa Chocky, tayari limeandaliwa onyesho litakalo wapambanisha Muumin, Chocky na Nyoshi Mei 19 ndani ya Escape One, Mikocheni jijini Dar es Salaam.

No comments