Habari

VIDEO: MUUMIN ASEMA WACHA CHOCKY ALE MATUNDA YA KIRANGA CHAKE TWANGA PEPETA …aibua shutuma kwa wanamuziki wa Twanga, amfagilia Asha Baraka

on

Mwinjuma Muumin anayemiliki bendi ya Double M Plus, amesema alicheka kwa dharau aliposikia Ally Chocky amesimamishwa kazi Twanga Pepeta.
Muumin akaenda mbali zaidi kwa kusema hayo ndiyo matunda ya kiranga cha gwiji mwenzake.
“Wakati magwiji tunafufua bendi zetu, mwenzetu ndiyo kwanza anavunja bendi yake na kwenda kuajiriwa”, mtu wa namna hii huna haja ya kumpa pole zaidi ya kumshangaa,” alisema Muumin.
“Kurudisha mpira kwa kipa sio jambo baya lakini sio kwenda kuweka kambi kabisa,” anaendelea kusema Muumin.
“Kama Chocky angesaini mkataba wa mwaka mmoja Twanga ningemwelewa, lakini miaka mitatu ni kuchuja kisanii na matokeo yake ndo hayo ya kusimamishana kazi kwa njia ya meseji, heshima iko wapi!”, alishangaa Muumin katika maongezi yake na Saluti5.
Muumin maarufu kama “Kocha wa Dunia” akasema kikubwa kinachomtafuna Chocky ndani ya Twanga sio Asha Baraka bali ni wasanii chipukizi waliopata umaarufu kupitia nyimbo alizoimba au kutunga Ally Chocky.
“Kwa dharau zilizopo kwa baadhi ya wanamuziki wa Twanga, nilijua tu kwamba Chocky hatapata amani pale. Nakumbuka nilivyoteseka mimi pale.
“Ukiacha kiongozi wa bendi mwenywe na wale wapiga vyombo baadhi hasa wapiga magita, lakini baadhi waimbaji pale wana chuki binafsi kama wimbo wake mwenyewe Chocky aliotunga. Hawajiamini, akienda mwanamuziki staa pale wanakuwa na roho mbovu,” anasimulia Kocha wa Dunia.
Muumin anazidi kueleza: “Nishawahi kushuhudia siku moja Chocky kanuna pembeni, analazimishwa avae sare na ‘stage master’ bwana James Kibosho. Sasa ukiangalia vijana wote pale ni watoto aliowalea mwenyewe Extra Bongo au waliopitia Double M huku, ni wadogo zetu wa mbali sana. Lakini leo unakwenda pale mtu anataka wewe aku-command sasa.
“Maana nina uhakika kabisa Asha Baraka hana roho hizo za ajabu, ana mheshimu Chocky kwasababu Chocky ameitoa mbali bendi ile pamoja na kuhama kwake, lakini kuna wanamuziki ambao wameingia pale sasa hivi, kutunga nyimbo kwenyewe mbinde, kuimba mbinde lakini wamekuwa na roho za ajabu.
 “Wanakuwa na chuki kwanini anakwenda pale mtu kama Chocky au Muumin, akifika pale wao wananuna na ndicho kilichowatoa Kupaza na Dogo Rama baada ya Chocky kuingia pale kwasababu tu ya chuki binafsi wameona kwanini huyu mkongwe karudi sasa sisi hatutasikika tena.
“Kwahiyo ushauri wangu ndugu yangu bora aje kwangu nije kumuajiri Double M, mimi nitampa heshima kuliko dharau anayoonyeshwa pale na watoto wadogo. Lakini narudia tena kwamba hiki ni kisa cha kujitakia, ni kiranga chake mwenyewe na mwenye kiranga huwa hapewi pole”.
Msikilize Muumin hapo chini

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *