WAAMUZI WANAWAKE WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA MAFUNZO YA UKOCHA

WAAMUZI wa soka wa kike nchini wamehimizwa kujitokeza kwa wingi pindi inapotokea fursa ya mafunzo ya kuwajengea uwezo na kwa mujibu wa kanuni za mchezo huo.

Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa chama cha waamuzi nchini (FLAT), Charles Ndagala.

Alisema kuwa FLAT inaendelea kuhamasisha wanawake kutoka taasisi, shule, mtaani na watu wa kawaida kujifunza kozi za uamuzi kwa ngazi mbalimbali ambazo pia zitaongeza idadi ya waamuzi wa kike nchini.

“Lengo linguine ni kuongeza ushiriki mkubwa wa wanawake ili waweze kuchezesha mechi mbalimbali za ndani na nje ya nchi.”

“Tutaendelea kuhamasisha wanawake kwa wingi kutokana na kuwa tayari tuna mifano mizuri ambayo tumeweza kusonga mbele,” alisema Ndagala.

Alibainisha kuwa mwitikio ni mkubwa kwa wanawake kuanzia ngazi ya Wilaya na kozi mbalimbali zimetolewa.


Katibu huyo amesema kuwa wanawake watapata fursa ya kuchezesha mechi za ndani na nje ya nchi kutokana na viwango vyao vitakapoonekana ambapo vitatumika kwa ndani na nje ya nchi.

No comments