WACHEZAJI HAWA WANASTAHILI TUZO YA WACHEZAJI BORA WA YANGA MSIMU HUU

TIMU ya Yanga ni kama imeshatawazwa rasmi kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya tatu mfululizo, baada ya jana kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Toto Africa.

Licha ya Yanga kufanikiwa kutetea taji la ubingwa wa Ligi Kuu kwa mara ya tatu mfululizo, bado msimu huu utabaki kuwa kati ya misimu yenye changamoto nyingi kwao, hasa kutokana na matatizo ya kiuchumi yaliyoikumba klabu.
Pamoja na matatizo yote ya klabu, kuna baadhi ya wachezaji wamekuwa na kiwango bora kuanzi mwanzoni mwa msimu hadi sasa na kuwa na mchango wa moja kwa moja ndani ya timu.

Hapa tunaleta wachezaji ambao wanastahili kuondoka na tuzo ya wachezaji bora wa Yanga msimu 2016/2017.

Thabani Kamusoko

Amekuwa msaada mkubwa kwenye eneo la kiungo, licha ya kutofikia ubora aliokuwa nao msimu uliopita, ila bado msimu huu amesimama kama mmoja wa wachezaji bora ndani ya Yanga.

Mziimbabwe huyo ameifanya Yanga kuimalika zaidi katikati ambapo amekuwa akicheza, ameifanya timu kuwa na uwiano mzuri kuanzia sehemu ya ulinzi na ushambuliaji.
Haruna Niyonzima

Haruna Niyonzima

Licha ya kuanza msimu kwa kusuasua, Niyonzima ndiye aliyerudisha Yanga kwenye mbio za ubingwa. Ndiye kiungo aliyetengeneza nafasi nyingi za kufunga klabuni, ubunifu wake kwenye eneo la mwisho la mpinzani kumechangia magoli mengi kwa upande wa Yanga.

Obrey Chirwa

Amefunga magoli 18 ndani ya msimu huu, 11 ya Ligi Kuu, 5 Kombe la FA, 2 ya michuano ya Kombe la Afrika uwezo wake wa kufumania nyavu umefanya mashabiki wasahau Donald Ngoma, kwani pengo lake limezibwa na Chirwa.

Simon Msuva

Ndiye mchezaji aliyechangia alama nyingi ndani ya klabu yake, ana nafasi kubwa ya kuwa mchezaji bora klabu ni kwake, amefunga magoli zaidi ya 20 msimu huu, ikiwemo ufungaji bora wa Kombe la Mapinduzi Zanzibar na magoli yake 13 mpaka sasa kwenye Ligi Kuu na ndiye kinara.

No comments