WACHEZAJI WA NDANDA FC HATARINI KUGOMA KUSHINIKIZA KULIPWA MISHAHARA YAO

IKIWA kwenye hatari ya kushuka daraja msimu huu, timu ya Ndanda imeingia kwenye sura mpya baada ya harufu ya mgomo wa wachezaji kunukia kutokana na kutolipwa mishahara yao.

Klabu ya Ndanda inaripotiwa kutolipa mishahara ya wachezaji wake kwa miezi mitatu pamoja na mahitaji mengine.

Baadhi ya wachezaji wa timu hiyo wameweka wazi kuwa hawatakuwa tayari kuendelea kucheza ikiwa hali hiyo ya kukosa mishahara itaendelea ndani ya klabu yao.

“Ukweli ni kwamba kuna hali mbaya klabuni, hatujalipwa mishahara yetu wala kupewa mahitaji muhimu, sielewi mechi zijazo hali itakuwaje,” alisema Wilbert Mweta.

Ndanda FC inapambana isishuke daraja ikiwa kwenye nafasi ya 13 kwa pointi zake 30 baada ya kucheza mechi 28.

Mchezo unaofuata itacheza na Prison ya mkoani Mbeya ambapo inatakiwa kushinda ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutoshuka daraja.

No comments