WADAU WA SOKA WASIFU UWEZO WA KIPA YOUTHE ROSTAND WA AFRICAN LYON

WADAU mbalimbali wa soka nchini wameonekana kusifu uwezo mkubwa wa kipa wa African Lyon, Youthe Rostand ambaye ni raia wa Cameroon.

“Moja ya vitu ambavyo African Lyon inajivunia ni kuwa na kipa huyo mwenye uwezo wa hali ya juu akiwa katika milingoti ya goli lake,” amesema mdau mmoja aliyefahamika kwa jina la Jumanne Lukwale.

Lukwale amesema kipa huyo raia wa Cameroon amekuwa mwiba kwa washambuliaji anaposimama langoni kwa kuokoa makombora makali huku akiwa na staili yake ya kupoteza muda timu yake inapokuwa mbele kwa ushindi.

Shabiki mwingine aliyejitambulisha kama Said Juma amesema urefu wake, mwili uliojengeka umekuwa ukiongeza ugumu kufungika na kwa hakika anayemfunga ni lazima awe amefanya kazi ya ziada na si kumfunga magoli rahisi na ya kizembe.

Kabla hajaangukia kwa kipa Mghana Daniel Agyei, Simba ilikuwa na mpango wa kumsajili kipindi cha dirisha dogo.

No comments