WASHAWASHA CLASSIC MIN BAND SASA YAPELEKA UHONDO BAGAMOYO

BAADA ya kuanza kukubalika na kuwa gumzo kubwa jijini Dar es Salaam na vitongoji vyake, sasa bendi mpya ya mipasho ya Washawasha Classic Min Band imeamua kuwapelekea raha mashabiki wake waishio Bagamoyo Pwani.

Mei 20, mwaka huu, bendi hiyo iliyo chini ya mpapasa kinanda mahiri, Amour Maguru imepanga kuwasha moto mkali ndani ya Mageti Mia Hall, kabla ya kesho yake kuhamia Machokodo Bar.

Taarifa kutoka ndani ya bendi hiyo zinasema kuwa, shoo zote hizo zimepangwa kuanza kurindima kuanzia majira ya saa 3:00 usiku na kuendelea hadi majogoo kwa kiingilio cha sh. 5,000 tu huku mastaa kibao wakitajwa kupamba.


Washawasha Classic inayoinukia kwa kasi kubwa hivi sasa, inakusanya nyota wengi wa muziki huo wakiwemo waimbaji Mwanahawa Chipolopolo, Omary Sosha, Amrah Maguru pamoja na Semeni.

No comments