WEMA SEPETU ATHIBITISHA KUTORUDIANA NA DIAMOND PLATNUMZ... awataka mashabiki wake wamuombee apate mume bora

MALKIA wa filamu na mitindo Bongo, Wema Sepetu amesema kuwa Diamond hivi sasa ni baba wa watoto wawili hivyo hawezi kufufua uhusiano wao uliovunjika siku nyingi.

“Jamani Diamond ni mume wa mtu sasa, ni baba wa watoto wawili. Kama kweli mnanijali basi mniombee nipate mume bora,” aliandika dada huyo kwenye akaunti yake ya Instagram.

Mrembo huyo aliyasema hayo wakati akijibu maswali ya mashabiki waliokuwa wakimuhoji kwa njia ya mtandao.


Mahusiano baina ya Diamond na Wema yaliteka hisia za mashabiki kabla ya kuvunjika kwa penzi lao.

No comments