WIMBO MPYA WA DARASA WAMNOGEA LAUDIT MAVUGO WA SIMBA SC

MSHAMBULIAJI nyota kikosi cha Simba raia wa Burundi, Laudit Mavugo ameonyesha dhahiri kuvutiwa msanii wa bongofleva, Darasa baada ya kuumwagia sifa kemkemu wimbo wake mpya uitwao "Hasara Roho."

Mavugo amesema wimbo huo anaupenda kutokana na mashairi yake yaliyopangiliwa vizuri huku akiongeza kuwa kuna mstari mmoja unamfurahisha sana akiusikiliza.

Mavugo ameamua kuandika moja ya mashairi ya wimbo huo katika kaunti zake za mitandao ya kijamii na amesema licha ya kutofahamu maana halisi ya wimbo huo lakini haimzuii kuupenda na kuusikiliza kila wakati.


“Huwa namfuatilia sana Darasa na ngoma yake ya “Muziki” ndiyo nilianza kuipenda na kuisikiliza huu wa sasa ambao umezidisha kufanya kumpenda Darasa kwa sababu kuna mstari umetokea kunifahamisha,” amesema Mavugo.

No comments