MWANAHAWA CHIPOLOPOLO YU NJIANI KUACHIA WIMBO MPYA "SINA JEMA"


UJIO mpya wa mwanamipasho gwiji wa kike, Mwanahawa Chipolopolo, ambao ni kibao kinachokwenda kwa jina la ‘Sina Jema’, umeanza kunadiwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Mwanahawa Chipolopolo kwa sasa anaitumikia bendi ya mipasho ya Washawasha Classic Min Band iliyo chini ya mpapasa kinanda mahiri wa taarab, Amour Maguru ambaye ndio mume wa staa huyo wa kike kwa sasa.

Kupitia akaunti zake za facebook, Instagram na Tweeter, mtunzi wa kibao hicho, Amrah Amour amesema kuwa kibao hicho kiko njiani na muda wowote kuanzia wiki ijayo kitawekwa bayana kwa mashabiki.

Amrah ametamba kuwa ni ‘Sina Jema’ ni kati ya kazi ambazo anaamini zitazidi kuinua chati ya Chipolopo pale kitakapotoka kutokana na meseji yake kuwa ya kipekee huku mapigo yake nayo yakiwa ni yanayochezeka zaidi.


No comments