WIZKID:MUZIKI KWANZA MAPENZI NA NDOA BAADAE

RAPA Wizkid amesema kuwa kwa hivi sasa anajikita katika fani yake ya muziki lakini masuala ya ndoa hayako kwenye akili yake.

Nyota huyo alisema kwamba tayari ameshapata watoto wawili ambao amezaa na wanawake wawili tofauti hivyo haoni haja ya kukimbilia kwenye ndoa.

“Ndoa si jambo la kukimbilia, nina watoto wawili nalea hivi sasa. Akili yangu inawaza muziki tu, wakati ukifika kila kitu kitakuwa wazi,” alisema rapa huyo.

“Sio kwamba sitaoa katika maisha yangu yote, hapana. Hivi sasa kipaumbele changu ni muziki tu.”


Rapa huyo ana watoto wawili wa kiume ambao alizaa na wanawake wawili tofauti.

No comments