WOLPER ASEMA AMETENGANA NA HARMONIZE LAKINI ATAENDELEA KUPIGA MZIGO KAMA KAWA NA WASAFI CLASSIC

MSANII wa filamu hapa nchini, Jacquline Wolper amesema kuwa hata baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake, Harmonize bado ataendelea kufanya kazi na kundi la “Wasafi” kama kawaida.

Staa huyo amesema alilifahamu kundi hilo kabla ya kuanza kuhusiana kimapenzi na Harmonize ambae hivi sasa wameshatengana.

“Huwa sipendi sana kumzungumzia ila ukweli ni kwamba niliijua Wasafi hata kabla ya kuanza kuhusiana na Harmonize,” alisema Wolper.


Penzi la wawili hao ilivunjika baada ya Harmonize kuripotiwa kumpa ujauzito msichana mwingine.

No comments