YANGA KUMKATA MSHAHARA NGOMA ENDAPO ATAKIUKA RUHUSA YA SIKU SABA ALIYOPEWA KWA AJILI YA MATIBABU YAKE AFRIKA KUSINI

MSHAMBULIAJI wa Yanga Donald Ngoma yuko nchini Afrika Kusini kwa matibabu ya maumivu yake ya mguu lakini akakumbana na kibano kutoka kwa Katibu Mkuu wa timu hiyo, Charles Mkwasa.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga ni kwamba safari ya Ngoma kutua nchini Afrika Kusini ina baraka zote za kiungozi baada ya mshambuliaji huyo kuitangulia kupewa ruhusa hiyo kwa benchi la ufundi kisha kwa Katibu mkuu Mkwasa. 
  
Bosi mmoja wa Yanga amesema, katika ruhusa hiyo ya Ngoma, Mkwasa amembana mshambuliaji huyo kutakiwa kuheshimu muda wa siku saba aliopewa katika matibabu hayo.

Mkwasa amembana Ngoma akimwambia kwamba endapo ataongeza muda huo katika matibabu hayo afrika Kusini, atakumbana na rungu la adhabu kutoka kwa klabu hiyo endapo huenda akakatwa mshahara wake kwa utoro.

“Ni kweli Ngoma yuko nchini Afrika Kusini kwa matibabu ya mguu wake unaomsumbua kwa muda mrefu na hili lina Baraka zote za uongozi kuanzia benchi la ufundi mpaka sekretarieti.”


“Ngoma ameambiwa wazi na Mkwasa kwamba amepewa ruhusa hiyo ya siku saba lakini endapo atazidisha muda huo atakumbana na adhabu ya utoro kwa kukatwa mshahara wake akifanya makosa hayo.”

No comments