YANGA SC YANUSA REKODI YA KIPEKEE LIGI KUU BARA... Simba kujifariji kwa Kombe la FA

LIGI Kuu Tanzania Bara inaelekea ukingoni ambapo kuna wastani wa mechi mbili kabla ya kufikia tamati huku mabingwa watetezi Yanga wakionekana kutokamatika baada ya kutoa vipigo mfululizo.

Itakuwa ni mara ya tatu kwa klabu ya Yanga kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara ambapo ni rekodi ya kipekee kwenye michuano hiyo inayotoa tiketi ya kushiriki kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Ilianza kwa kusuasua wakati wa mzunguuko wa kwanza kiasi cha kuachwa kwa jumla ya pointi nane na watani wao wa jadi, Simba, lakini hivi sasa kila kitu kimebadilika na kuonekana kuwa na dhati ya kutetea taji hilo.

Pamoja na matatizo ya kiuchumi waliyokuwa wakikabiliana nayo, Yanga wanaelekea kuweka rekodi ya kuchukua taji hilo kwa mara 28, zaidi ya timu yoyote ile kwenye historia ya Ligi Kuu Bara.


Watani wao wa jadi, Simba faraja pekee waliyokuwa nayo ni baada ya kutinga fainali ya michuano ya Kombe la FA, lakini ubingwa wa Ligi Kuu Bara umeendelea kuwa ndoto isiyotimia.

No comments