YANGA YAICHAPA MBEYA CITY NA KUREJEA KILELENI LIGI KUU


Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom, Yanga, wameitungua Mbeya City 2-1 kwenye mchezo mkali uliochezwa Uwanja mkuu wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kwa matokeo hayo, Yanga imerejea kileleni mwa msimamo wa Ligi na kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea taji lao.

Yanga imeabakiza michezo miwili huku wapinzani wao Simba wakiwa wamebakiza mchezo mmoja tu.

Mabao ya Yanga yamefungwa na Simon Msuva dakika ya 7 na Obrey Chirwa dakika ya 67 wakati lile la Mbeya City lilifungwa na Haruna Shamte dakika ya 57.

Hata hivyo Yanga walipata piga baada ya Msuva kutolewa dakika ya 8 kufuatia kuumia kichwani wakati anafunga goli lake, nafasi yake ikachukuliwa na Juma Abdul.

Yanga itarejea tena Uwanjani Jumanne kucheza mchezo wake wa kiporo dhidi ya Toto Africa ya Mwanza.  

No comments