YANGA YAWEKA MIKAKATI YA KUMUUMBUA MNYAMA

YANGA imeapa Miungu yote kwamba kama kuna kipindi Simba imekuja mbele yao vibaya basi ni katika fainali ya Kombe la FA na kwamba iwe jua iwe mvua watani wao hao hawatatoka salama baada ya kuwekewa mkakati mkubwa.

Mikakati hiyo ya Yanga imesukwa kuanzia jana kabla ya mchezo wa Mbao FC wakiazimia mambo kadhaa ya kujipanga katika mchezo huo ambao utafanyika mwishoni mwa msimu.

Vigogo wa Yanga ambao wapo katika Kamati ya Utendaji na Kamati ya mashindano, wamekutana jijini Mwanza na kufanya maamuzi makubwa, ya kwanza kuibakiza timu hiyo mjini Geita.

Hawakuisha hapo, vigogo hao wakakutana na kocha wa timu hiyo, George Lwandamina na kumpa mkakati wao kwamba katika mchezo wa fainali endapo watakutana na Simba wanataka kuwaachia maumivu ya kipigo na hawataki kupoteza mechi dhidi ya wekundu hao kwa mara ya tatu mfululizo.

“Tumefanya kikao cha kwanza kutafakari kama tutakutana na Simba, tumekubaliana kwamba safari hii tutulie na kujipanga kwani hatutaki kumkosa myama,” alisema kigogo huyo.

“Tumekubaliana kwamba tuwaondoe wachezaji wasioaminika na huo mpango ameshafikishiwa kocha tumemwambia afanye kazi yake kwa utulivu lakini mipango yake ya ushindi ianze sasa."  

Tukimaliza mchezo wetu na Mbao tumekubaliana na timu ibaki Geita itulie huko ikirudi huku tunataka kuona hakuna kuwaacha huru kwa muda mrefu unajua hawa wenzetu wana mambo mengi nje ya uwanja.

No comments