YOUNG KILLER AFICHA UJIO WAKE MPYA MBELE YA MASHABIKI

RAPA Young Killer Msodoki baada ya kufanya vizuri na wimbo "Sinaga Swagger" amedai hataki mashabiki wajue atakuja vipi katika project yake inayofuata.

Wimbo uliopita wa rapa huyo ulizua gumzo mtaani na katika vyombo mbalimbali vya habari baada ya kuwachana baadhi ya wasanii wenzake.

Akiongea na saluti5, Young Killer amedai tayari ameandaa kazi nyingine kwa ajili ya ujio wake mpya lakini hataki mashabiki wajue kama ataendelea na ngoma za kuwachana wasanii wenzake au la.

Baaada ya Sinaga Swagger kuwachana wale wana kiukweli kabisa nina project nyingi kali na muda wowote au saa yoyote naweza kubadilisha matokeo kwa sababu kuna nyimbo nyingi ndani kali hata sijajua ninazitoa lini au saa ngapi.


"Watanzania wategemee vitu vizuri na kwa mtindo wowote,” alisema msodoki.

No comments