YUSUPH MANJI AUNDA KIKOSI CHA USAJILI YANGA BAADA YA KUMALIZA "MAMBO YAKE BINAFSI"

MWENYEKITI wa Yanga, Yussuph Manji amemaliza mambo yake lakini katika kuelekea katika usajili wa kikosi hicho jeshi maalumu la vigogo limeundwa kuhakikisha linamaliza mambo ya usajili wa kikosi hicho mapema kabla ya Ligi kumalizika.

Taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ni kwamba kikundi cha vigogo wasiopungua watano kimeundwa kuanza jukumu hilo la kufanya usajili wakianzia na kuongeza mikataba ya wachezaji ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu.

Mbali na hilo, pia habari njema ni mkwamba tayari mwenyekiti wa klabu hiyo, Manji wakati wowote kuanzia wiki ijayo atashirikiana haraka na Kamati hiyo kuunda kikosi cha nguvu kwa msimu ujao.

Kikosi hicho kinakusudiwa kuwa na sura ya ushawishi mkubwa kikiwakusanya Seif Ahmed,Abdallah Bin Kleb, Mustafa ulungo na Samuel Lukumay wakifanya kazi na katibu mkuu wa timu hiyo, Charles Mkwasa ambaye kitaaluma ni kocha.

Tayari Kamati ya mashindano imeshapokea ripoti ya awali kutoka kwa kocha wao George ambaye katika kumalizia ataikabidhi rasmi kwa Mkwasa kabla ya kuikabidhi kwa Kamati ya mashindano.


“Usajili utakamilika katika muda mfupi ujao na tunachotaka kufanya ni kumaliza mambo mapema hata kabla ya Ligi kumalizika, tunataka kufanya mambo makubwa kwa kuunda timu yenye nguvu,” alisema bosi huyo.

No comments