ZAHIR ALLY ZORO ATOA SALAMU ZA POLE KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO

MKONGWE wa muziki wa dansi, Zahir Ally “Zorro” ametoa salamu za pole kwa Watanzania ambao majengo yao yameingiliwa na mafuriko, hususan maeneo ya Bweju, Tanga na sehemu nyingine mbalimbali hapa nchini.

Katika salamu hizo, Zorro amesema kuwa maafa yaliyowafika watu wa maeneo hayo ni ya Watanzania wote kwa kuwa sote ni ndugu na kuwaomba wawe na subira katika kipindi hiki kigumu cha mpito cha maafa hayo.


“Unajua, natural calamity hainaga ubingwa. Landslides maeneo ya Mombo kama kawaida. Lakini mwaka huu yamezidi, barabara zimefunikwa kwa kiasi kikubwa. Poleni madereva pia wa Tanzania hii,” amesema mkongwe huyo.

No comments