ALLY CHOCKY AISHUTUMU CHAMUDATA TAARIFA ZA KIFO CHA TONGOLANGA


Mwimbaji supastaa wa Twanga Pepeta Ally Chocky amekishutumu Chama Cha Muziki wa Dansi Tanzania (Chamudata) kwa namna kilivyoshindwa kujiongeza katika upashaji habari wa kifo cha mwanamuziki Harila Tongolanga.

Akiongea na kipindi cha Weekend Bonanza cha Clouds FM jana usiku, Chocky pia alizungumzia namna Tongolanga aliyefariki wiki iliyopita, alivyokuwa balozi mzuri wa muziki wa kiasili.

Msikilize Chocky hapo juu namna alivyoongea na Clouds FM juu ya Tongolanga.

No comments