AMIN WA THT AFICHUA SABABU YA UKIMYA WAKE KWENYE GEMU LA MUZIKI

MWIMBAJI wa kundi la THT, Amin amesema kuwa sababu za ukimya wake wa muda mrefu ni kutokana na kuwa bize akiandaa kazi mpya ili kuwaletea mashabiki wake kitu kilicho bora zaidi.

Msanii huyo alidai kuwa watu wametafsiri vitu tofauti huku wakidhani kwamba maisha ya ndoa yamemfanya kujiengua na sanaa jambo ambalo si kweli.

“Kitu ambacho si kweli, soko la muziki wa sasa ni gumu na inakulazimu kutumia muda mrefu ili kuandaa kazi yenye ubora na sio kama ilivyokuwa wakati tunaanza sanaa,” alisema msanii huyo.

“Ndoa yangu haijachangia lolote juu ya ukimya wangu isipokuwa ni mpango wangu wa kutuliza akili kabla ya kuachia kazi mpya,” aliongeza msanii huyo.

No comments