ANDRE AYEW AGOMA KUONDOKA WESTHAM UNITED

STRAIKA wa Westham United, Andre Ayew ameweka bayana azma yake ya kutaka kuendelea kukipiga katika klabu yake hiyo ya sasa, licha ya kupokea ofa nyingi kutoka katika timu mbalimbali barani Ulaya.

Kauli ya nyota huyo wa zamani wa Swansea inafuatia tetesi za hivi karibuni zinazodai kuwa anatakiwa na timu za Juventus na Nice.

Akiweka wazi dhamira yake ya kubakia westham, Ayew amesema amefurahishwa na hali ya mambo ndani ya klabu yake hiyo hivyo hana mpango wa kuondoka kwa wakati huu.

Straika huyo ana kandarasi ya kubakia Westham, United hadi mwishoni mwa msimu wa mwaka 2019 na kwamba anaamini anaweza kurefusha mkataba huo.

Akinukuliwa, Ayew alisema: “Huu si wakati wa kuzungumzia suala la mimi kuondoka hapa, kwasababu nina mwaka mmoja na nusu ndani ya kandarasi yangu.”

“Pamoja na hilo, ninajisikia faraja na furaha kuwa katika klabu ambayo inanithamini na kunipa nafasi kubwa ya kucheza katika kikosi cha kwanza.”

“Nitabaki hapa hadi pale nitakapozungumzia suala hili baada ya kumalizika kwa mkataba nilionao hivi sasa,” alisisitiza straika huyo ambaye pia yumo katika kikosi cha timu ya taifa ya Ghana.


Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Nice ya Ufaransa, zinasema kuwa imepanga kutumia kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kufanya usajili wa majira ya joto, huku ukiweka jina la Ayew katika orodha ya wachezaji inayowawania.

No comments