ANTOINE GRIEZMANN ASEMA BADO YUPOYUPO SANA TU ATLETICO MADRID

STRAIKA wa timu ya Atletico Madrid, Antoine Greizmann amezisikia taarifa za kutaka kuondoka na sasa amekanusha akisema bado yupoyupo kwanza katika La Liga.

Amesema hayo huku kukiwapo na tetesi kwamba ana mpango wa kuhamia katika moja ya klabu kadhaa barani Ulaya.

Klabu za Manchester United, Bayern Munich pamoja na Manchester City zinatajwa katika orodha ya timu zinazomwania.

Antoine Griezmann anayeitumikia pia timu ya taifa ya Ufaransa mkataba wake unafikia tamati majira ya mwaka 2021 ndani ya kikosi cha Atletico, amekanusha tetesi zote hizo kwa kusema bado yuko sana ndani ya Ligi ya La Liga akiitumikia Atletico.

Hatua hiyo inazifanya klabu mbalimbali za Ulaya zinazotaka kupata saini yake kugonga mwamba.
Hatua hiyo pia imeelezwa kuongezewa uzito baada ya Atletico Madrid kutumikia adhabu ya kutosajili wachezaji waliyopewa na FIFA.

Straika huyo aliyeng’ara katika fainali za Mataifa ya Ulaya ya mwaka 2016 amesema kwa sasa anataka kutuliza akili zake akiwa katika klabu yake ya sasa ya Atletico Madrid.

“Uvumi wote huu ni jambo linguine ambalo sijaliweka katika kipaumbele change, nitaendelea kufikia haya,” amesema Griezmann.

“Ninichoweza kusema ni kwamba ninaamini tuna kikosi kizuri kwa ajili ya misimu yote nikiwa hapa.”

No comments