ANTONIO CONTE APEWA RUNGU LA KUMTUPIA VIRAGO DIEGO COSTA


ANTONIO CONTE ameungwa mkono na bodi ya Chelsea baada ya kumtupia virago mshambuliaji Diego Costa kwa kutumia ujumbe wa simu.

Wiki iliyopita, Costa alianika kwa vyombo vya habari kwamba kocha huyo Mtaliano alimtumia ‘meseji’ kumweleza kuwa si sehemu ya mipango yake kwa msimu ujao.

Katika meseji hiyo ambayo kwa mara ya kwanza ilianikwa hadharani na gazeti la AS la Hispania, Conte aliandika: “Hi Diego, natumaini umzima. Shukrani kwa msimu tulikuwa pamoja. Nakutakia heri kwa mwaka ujao, lakini wewe si katika mpango wangu.”

Conte alitarajiwa kukatiza likizo ili kufanya kikao na mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich na mwenyekiti Bruce Buck kutokana na kumpiga chini Costa bila kuwashirikisha, lakini sasa gazeti la Sun limefichua kuwa viongozi wa klabu wametuma ujumbe wa wazi kwa timu, kwamba wanaunga mkono uamuzi uliochukuliwa na kocha huyo.

Mtaliano huyo ambaye yuko mapumzikoni nyumbani kwao Italia, anatarajiwa kurudi Stamford Bridge siku chache kabla kuanza maandalizi ya msimu Julai 7.

No comments