ARSENAL SASA YAHAMISHIA MBIO ZA USAJILI KWA ANTHONY MARTIAL WA MANCHESTER UNITED


Arsene Wenger amemuorodhesha winga wa Manchester United Anthony Martial katika orodha yake ya washambuliaji anaotaka kuwanunua kiangazi hiki.

Kocha huyo wa Arsenal ameanza kumkatia tamaa kinda wa Monaco Kylian Mbappe na sasa anampigia hesabu  Martial. 

Wenger anajiandaa kulipa pauni milioni 40 kwa Martial, ambaye amekosa nafasi ya kudumu Old Trafford chini ya Jose Mourinho. 

Hata hivyo Wenger anahofia kuwa Mourinho anaweza kumbania kutokana na uhasimu mkubwa ulioko kati yake na kocha huyo wa Manchester United.

No comments